Recent comments

Breaking News

Shetta akiri kutumia mtindo wa Black Rhino kuteka soko na sasa anaingiza zaidi ya milioni 5 kwa show

Shetta akiri kutumia mtindo wa Black Rhino kuteka soko na sasa anaingiza zaidi ya milioni 5 kwa show
Mara nyingi huwa vigumu kwa rapper mkubwa wa Tanzania kukubali kuwa alirap kwa kufuata mtindo wa rapper mwenzake wa hapa Tanzania na mwisho kuingiza pesa hata zaidi ya aliyemuiga. Wengi watakwambia mimi namfuatilia sana Jay-Z, Lil Wayne na wengine.
Hiyo imekuwa tofauti kwa baba yake Qayllah, Shetta ambaye amekiri kuwa alitumia mtindo wa rapper wa Choka Mbaya, Black Rhino na akapita ‘mulemule’.
Shetta amefunguka katika mahojiano aliyofanya na Jabir Saleh aka Kuvichaka kupitia The Jump Off ya 100.5 Times Fm akiwa kama mkali wa The Jump Off wa wiki.
“Umenikumbusha, Rhino pia ni mtu niliyekuwa namsikiliza, Rhino na Noorah sana. Ndio maana ukisikiliza nyimbo yangu ya kwanza nimefanya kama Rhino.” Amesema Shetta.
Mkali huyo wa Nidanganye alirap kidogo kuonesha kweli alipita mulemule kwa Rhino, “Hizo ‘sawaa’ nini zote zilikuwa vitu vya Rhino alikuwa anapenda kupita.”
Hata hivyo, Shetta alipoambiwa amemkopi kabisa Rhino na kuwa Rhino mwingine, ilimbidi atafute jinsi ya kuweka vitu vyake ili awe yeye.
“Nilikuwa namfeel, sasa baada ya kutoa ngoma ile watu wakasema ‘Rhino mtupu’ kwa hiyo nikawa najaribu ku-create kitu changu kingine, kwa sababu kweli ukisikiliza unasema yeah huyu Rhino huyu.”
Katika hatua nyingine, Shetta aliiambia Tovuti ya Times Fm kuwa hivi sasa anaingiza zaidi ya milioni 5 kwa kila show na amewahi kuvunja rekodi ya ukumbi wa Bilicanas kwa kujaza watu.
“Sasa hivi nimepandapanda kidogo, kuanzia sita M, nafanya…sita au tano. Muziki umebadilika kwa sababu sasa hivi watu wanaingiza hela. Kwa hiyo nasisitiza tunaangalia na ukubwa wa show, na nani kaja. Kuna rappers, lakini wanarap vipi? Katika midundo gani, muziki wao upo katika career gani? Mimi ni mfanyabiashara. Mimi nahisi kwenye ule ukumbi wa Bilicanas hakuna mtu ambaye amevunja rekodi kwa kujaza watu kwenye show. Kama mimi show yangu ya mwisho wenyewe walikuwa wanakiri. Show zinatokea zinaenda zinarudi lakini mimi nilivunja kwa sababu tiketi ziliisha watu walikuwa nje wanataka kuingia lakini wakawa hawaruhusu tena watu.
“Nina fans wengi, muziki wangu unaniruhusu kufanya hivyo. Rappers wengi wanaimba muziki ambao yaani ile kibiashara hauko sawa. Kwa hiyo wakija kwenye biashara sawa. Tunaweza tukasikia kuna mtu nae katangaza hivyo.”

No comments