Recent comments

Breaking News

Exclusive:- Haya ni mambo 10 muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu Notorious B.I.G

Mambo 10 muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu Notorious B.I.G
Wengi humuita mfalme wa Hip Hop/Rap kutokana na uwezo wake mkubwa aliounesha wa kurap enzi ya uhai wake, Christopher George Letore Wallace aka Notorious B.I.G, aliyewakilisha label ya Bad Boy na kuisimamia vyema Junior M.A.F.I.A Crew iliyomtambulisha zaidi Lil Kim aka Queen Bee.
Yapo mambo mengi yanayofahamika kuhusu rapper huyu aliyefariki kwa kupigwa risasi March 9, 1997 huko Los Angeles, Marekani lakini haya ni mambo 10 muhimu unayotakiwa kuyafahamu.
  1. Kuhusu familia yake
Christopher Wallace aka Notorious BIG, ni mtoto pekee wa mama yake Voletta Wallace ambaye alikuwa mhamiaji kutoka Jamaica, aliyemzaa BIG akiwa Brooklyn, New York. Voletta alikuwa mwalimu wa shule ya awali.
Baba yake anaitwa George Latore alikuwa mwanasiasa wa Jamaica. George aliiacha familia yake wakati BIG akiwa na miaka miwili tu, na hivyo mama yake akalazimika kujiingiza katika biashara ya kuuza mwili huku akiendelea na kazi ya ualimu ili aweze kumtunza BIG.
Alipewa jina la utani BIG kutokana na kuwa na mwili mkubwa wakati akiwa mdogo.
  1. Alisoma shule moja na wanafunzi wawili waliogeuka kuwa rappers wakubwa
Big alisoma shule moja na wanafunzi ambao waligeuka kuwa rappers wakubwa. Jay Z na Buster Rhymes. Jay Z pia alijikuta akiwa na historia ya familia inayotaka kufanana na ya BIG.
  1. Hakuwahi kupata chini ya A alipokuwa shule
Christopher Wallace alikuwa mwanafunzi mwenye akili na inawezekana kabisa maisha ndiyo yalizipoteza ndoto zake.
Mama yake mzazi alieleza kuwa mwanae hakuwahi kupata chini ya ‘A’ na kwamba alikuwa na ndoto za kuwa daktari wa meno au graphic designer kabla hajaachana na shule na kuingia mtaani. Aliwahi kushinda tuzo nyingi za kitaaluma wakati yuko shule hasa katika somo la Kiingereza alilokuwa analipenda zaidi. 
  1. Aliwahi kushtakiwa kwa kutumia jina la Biggie Smalls na kulazimika kubadili
Jina la Big Small limetoka kwenye filamu ya mwaka 1975 inayoitwa ‘Let’s Do It Again’. Katika filamu hiyo kulikuwa na kundi la waharifu linaloongozwa na mtu aliyeitwa Biggie Smalls na jina lake halisi ni Calvin Lockhat.
Christopher Wallace alipoanza kulitumia jina hilo kama jina lake kwenye rap game, alishitakiwa na Lockhart na kulazimika kubadili jina na kutumia Notorious B.I.G.
Hata hivyo, watu wake walidai kuwa jina la Biggie Small alipewa kwa utani kwa kuwa alikuwa anapenda kula nyama kubwa ya kuku na sio nyamba ndogo (Big, not Small).

  1. Alikuwa muigizaji na mchekeshaji
Mbali na kuwa rapper, Christopher Wallace ameshaonekana kwenye vipindi mbalimbali vya runinga enzi za uhai wake. Aliwahi kuonekana kwenye drama maarufu ya ‘New York Undercover’, na pia kwenye comedy show ya ‘Martin’.
Alikuwa amepanga kuonekana tena kwenye filamu nyingine akiwa anacheza kama muuza dawa za kulevya akiwa na Robert Deniro na Christopher Walken, lakini hakuweza kufanikisha kwa kuwa alikufa kabla.
kufanikisha kwa kuwa alikufa kabla.
  1. Alipanga kufungua mgahawa wa kuuza vyakula vya asili ya Afrika ‘Soul Food’
Jamaa alikuwa na mpango wa kufungua mgahawa ambao ungekuwa unauza vyakula vinavyoendana na utamaduni wa watu weusi (Afrika) wanaoishi Marekani, vyakula vinavyojulikana kama ‘Soul Food’. Wateja wake wakubwa walikuwa wale wa maeneo aliyokuwa anaishi na mama yake ‘Bedford-Stuyvestant.
Alipanga kuuita mgahawa huo “Big Poppa’s.”
  1. Alifungwa jela
BIG alikamatwa mwaka 1981, 1990 na 1991, na kufuatia matukio hayo, aliwahi kukaa jela kwa kipindi cha miezi tisa huko kaskazini mwa Carolina kwa kosa la kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
  1. Alipata ajali ya Gari
Wakati akiwa anaiandaa albam yake ya pili ‘Life After Death’, Biggie alipata ajali ya gari na kuumia mkuu wa kushoto. Hali hiyo ilimpelekea kukaa kwenye kiti kwa muda na kisha kulazimika kutumia mkwaju kwa ajili ya kumsaidia kutembea hadi alipofariki.
  1. Mashairi yake yanatumiwa kama ‘sample’ na rappers wakubwa
Baada ya kifo chake, mashairi yake yamekuwa yakitumiwa kama Sample au hata kurudiwa baada ya mistari na rappers wakubwa na waimbaji wa R&B na Pop kama vile, Jay Z, 50 Cent, Nas, Fat Joe, Nelly, Pharrel Williams, Lil Wayne, Ludacris, Big Pun, Usher, Ashanti, Alicia Keys na Nelly Furtado.
  1. Kuhusu Foundation iliyanzishwa kama kumbukumbu yake
Imeanzisha ‘Christopher Wallace Memorial Foundation’ ambayo inafanya party ya kila mwaka (B.I.G Night Out), yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili kununulia vifaa vya shule kwa ajili ya watoto na kuvigawa ili kumuenzi rapper huyo.
Kwa kuwa tukio hilo linakuwa kwa ajili yake, maana ya B.IG inabidilishwa na kuwa na ujumbe unaosema Vitabu badala ya bunduki (Books Instead of Guns).

No comments