Hackers wazishambulia tovuti za NATO, kundi la hackers wa Ukraine watangaza kuhusika
Jumamosi (March 15), wezi wa mitandao maarufu kama Hackers walizishambulia tovuti mbalimbali za Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO), na kusababisha tovuti hizo kutopatikana ipasavyo kwa masaa kadhaa.
Msemaji wa Nato, Oana Lungescu alieleza kupitia Twitter kuwa ingawa akaunti hizo zilishambuliwa na hackers hao hazikuathiri utendaji kazi za ujumla za NATO.
Kwa mujibu wa CNN, tovuti za NATO zilikuwa ‘down’ kwa masaa kadhaa na hata baada ya tamko la msemaji wa NATO ziliendelea kuwa katika hali hiyo kwa muda wa masaa matatu.
Ingawa NATO hawakueleza nani aliyehusika na kitendo hicho, kundi la hackers wa Ukraine linajulikana kama ‘Cyber Berkut’ lilitoa tamko kuwa limehusika na kwamba hiyo ni sehemu ya zoezi la kupinga uingiliaji wa NATO nchini Ukraine.
“Sisi, Cyber Berkut, tunatangaza kwamba leo saa kumi na mbili kamili jioni tumeanza kuushambulia vyanzo vya mitandao ya NATO. Sisi Cyber Berkut, hatutaruhusu uwepo wa NATO katika ardhi ya nchi yetu ya nyumbani, kwa sababu tunapinga uingiliaji wa NATO nchini Ukraine.” Walieleza hackers hao katika maelezo yao.
Jina la Cyber Berkut linafanana na jina la kundi la watu waliokuwa wanatumiwa na Viktor Yanukovych, rais wa Ukraine aliyeondolewa madarakani. Kundi hilo lilikuwa linaitwa ‘Berkut’
No comments