Nay wa Mitego kufanya collabo na Jose Chameleone, ataachia wimbo aliofanya na Diamond hivi karibuni.
Mwaka 2014 unaweza kuwa mwaka ambao mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Flava wanaweza kuwasikia collabo nyingi za wasanii wa Tanzania na wakali wa nchi nyingine.
Tushasikia uwepo wa collbao ya Steve RnB na Wyre Da Love Child iko jikoni, wakati Madee alishaitoa collabo yake na P-Unit wa Kenya, Chid Benz na Cannibal na bado orodha inaendelea.
Rapper wa Manzese, Nay wa Mitego ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa amepanga kufanya wimbo na mwanamuziki wa Kitamataifa, Jose Chameleone.
“Next Collabo…namatarajio ya kufanya ngoma na Chameleone.” Amesema Nay wa Mitego. “Bado haijakamilika, tuko kwenye Process.”
Katika hatua nyingine, Nay amesema kuwa project yake na Diamond ndio itakayofuata hivi karibuni, “soon as possible ngoma itaenda hewani.”
No comments