Recent comments

Breaking News

Exclusive: Jux asema aliandika 'Nitasubiri' akiwa na hisia za baada ya matatizo ya Jackie Cliff, msikilize hapa

Exclusive: Jux asema aliandika
Member wa kundi la Wakacha, Jux ambaye wiki hii ameachia wimbo alioupa jina la ‘Nitasubiri’ ambao tangu aweke wazi jina la wimbo huo wengi walianza kuhisi kuwa amemuimbia mpenzi wake Jackie Cliff, ameweka wazi chanzo cha kuandika wimbo huo.
Jux ameiambia tovuti moja maarufu hapa town kuwa hakuuandika wimbo huo kwa maana ya kuu-dedicate kwa Jackie Cliff, lakini ukweli ni kwamba hizo ndizo hisia alizokuwa nazo wakati anaandika wimbo huo na ilikuwa ni baada ya mpenzi wake huyo kupata matatizo nchini China.
“Ni kweli, sijadedicate kabisa kusema nini lakini kipindi ambacho nimerudi ilikuwa hayo mambo yameshatokea na vitu kama hivyo, kwa hiyo nilivyorudi nilikuwa na hiyo idea. Kwa hiyo naweza kusema ilikuwa hivyo kweli.” Jux ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Kweli kwa kipindi hicho ambacho nimerekodi hiyo nyimbo nilikuwa na feeling hiyo kichwani kwangu na kweli hayo matatizo yalikuwa yameshatokea kama ilivyotokea halafu nikarekodi hiyo nyimbo. Yaani naweza kusema hivyo kwa sababu ndio feeling ambayo nilikuwa nayo kwa huo muda na kitu kilikuwa ndio kishatokea hicho.” Ameongeza.
Ameeleza kuwa ingawa producer wa wimbo huo alimtaka afanye wimbo wa kuchezeka, yeye aliomba afanye kile anachokifeel kwa muda huo kwa kuwa nyimbo zake huendika kutokana na hisia za kweli alizonazo, lakini pia aliona huo ni wimbo wa tofauti sana kwake.
“Hapo kitu ambacho najaribu kusema sikuwahi kusema kwamba naimba hii nyimbo kwa ajili ya mtu fulani, no. Niliingia studio nikamkuta Bob, Bob akaniambia inabidi tufanye nyimbo. Tena Bob alitaka tufanye nyimbo ya kuchezeka. Nikamwambia Bob kitu ambacho kiko kichwani kwangu sasa hivi ambacho kikatoka kitu kizuri. Bob akaniambia yeah...nikamwambia hiki kitu mimi nakiona na inabidi niimbe kitu hiki. Bob akaniambia au unamuimbia nini, nikamwabia yeah...inaweza ikawa hivyo kwa sababu, ndio kitu ambacho nafeel right now.”


No comments