Je wajua:- Kuwa Notorious B.I.G hakuwahi kupata chini ya 'A' darasani, alikuwa na ndoto ya kuwa daktari
Christopher Wallace aka B.I.G au Biggie Small, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi March 9, 1997 hakuwa tu na sifa mbaya ya kuwahi kujiingiza kwenye biashara ya dawa za kulevya, bali aliwahi kuweka historia nzuri pia katika masomo yake kabla hajaachana na shule.
Rapper huyo alikuwa mwanafunzi mwenye akili na inawezekana kabisa maisha ndiyo yalizipoteza ndoto zake.
Mama yake mzazi, Volleta Wallace alieleza kuwa mwanae hakuwahi kupata chini ya ‘A’ na kwamba alikuwa na ndoto za kuwa daktari wa meno au graphic designer kabla hajaachana na shule na kuingia mtaani. Aliwahi kushinda tuzo nyingi za kitaaluma wakati yuko shule hasa katika somo la Kiingereza alilokuwa analipenda zaidi.
No comments