Tazama VIDEO ya Rihanna akimfuata Drake hadi msalani, atoka hotelini amevaa nguo za Drake, ni wapenzi rasmi
Wanasema penzi ni kikohozi… kama tunaamini huo msemo basi tunaweza kusema Rihanna amepaliwa na hawezi kuficha tena kuwa yeye na Drake ni zaidi ya marafiki bali wapenzi waliokolea.
Hivi karibuni wawili hao wameambatana katika ziara ya Drake barani Ulaya ‘Would You Like A Tour?’ na wameonekana kuwa na ukaribu uliopitiliza.
Wakati wanatoka hotelini huko Manchester, Rihanna alionekana akiwa amevaa nguo ambazo zilivaliwa na Drake awali hivyo kuonesha kabisa kuwa hawa ni zaidi ya marafiki. Inawezekana
Wiki hii, wawili hao walienda sehemu ambayo walitulia na kupata mvinyo, lakini baada ya muda Drake aliamka na kuelekea msalani.
Katika hali isiyo ya kawaida, Rihanna alionekana akimfuata Drake msalani na kuingia kwenye ‘choo’ cha wanaume hali iliyowafanya watu kupiga kelele na kuzungumza huku mtu mmoja akichukua video kwa simu ili kuutunza ushahidi.
No comments