Huyu ndio mchezaji atakayekuwa akilipwa fedha nyingi baada ya Ozil Arsenal
Baada ya kufanya vizuri sana katika klabu ya Arsenal msimu huu, uongozi wa klabu hiyo sasa upo tayari kumuongeza mkataba mpya kiungo Aaron Ramsey.
Kwa mujibu wa taarifa zilizogaa kwenye vyombo vya habari nchini Uingereza mkataba mpya wa Ramsey utamfanya awe mchezaji wa anayelipwa vizuri katika klabu ya Arsenal.
Ramsey, 23, anatarajiwa kupewa mkataba wa miaka mitano, utakaomfanya apeleke benki kiasi cha pound 100,000 kwa wiki. Hatua hii inakuja baada ya kuwa na msimu mzuri na Arsenal akiwa tayari mpaka sasa ameshaifungia mabao 13 timu hiyo, akishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal mara 4 mfululizo.
Ni Mesut Ozil pekee atakayemzidi Ramsey kwa mshahara – dili hilo litamfanya mchezaji huyo raia wa Wales kuingiza fedha mara mbili anayoingiza sasa.
No comments