Hii ndio rekodi mpya ya mabao aliyoiweka Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo ameandika historia mpya katika soka jana usiku kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Cameroon ambapo Ureno walishinda mabao matano kwa moja.
Ronaldo ambaye alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo yaliyomfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya timu hiyo ya taifa.
Winga huyo wa Real Madrid sasa amefikisha jumla ya mabao 49, mawili zaidi ya Pauleta ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya kufunga mabao huko nyuma.
Akizungumza baada ya mchezo, Ronaldo alisema: ‘Sina wasiwasi kuhusu kuvunja rekodi, ni kitu ambacho kinatokea tu ukiwa unajituma sana.”
No comments