Elikem na Pokello wa 'Big Brother Africa' wakanusha taarifa za kuachana
Washiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' waliodumu kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda, Elikem na Pokello wamekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao kuwa wamepigana chini.
Tarifa za kuachana kwao zilidai kuwa chanzo ni Elikem kumpa ujauzito mwanamitindo ambaye anafanya shughuli zake nchini Ujerumani.
Pokello alikuwa wa kwanza kukanusha habari hizo kupitia Twitter na kudai kuwa endapo wataachana watatoa taarifa wao wenyewe.
Elikem alifuatia kwa kutweet kuonesha kuwa hakuna hata mgogoro kati yao.
"Pokello na mimi bado tuna furaha pamoja ,ni nini tumewakosea ,nampenda mke wangu." Alitweet Elikem
No comments