Mchezaji wa Bayern Munich Frank Ribery kuukosa mchezo dhidi ya Arsenal
Zikiwa zimebaki siku kadhaa kabla ya raundi ya kwanza ya mechi za mtoano wa ligi ya mabingwa wa ulaya, mabingwa watetezi Bayern Munich wamethibitisha kwamba mchezaji wao tegemeo Frank Ribery ataukosa mchezo wa kwanza dhidi ya Arsenal baada ya kufanyiwa upasuaji wa makalio.
Winga huyo wa kimataifa, 30, hakuwepo kwenye mchezo wa ushindi wa 2-0 dhidi ya Nurnberg siku ya jumamosi kutokana na majeruhi na ikabidi apigwe kisu siku ya Alhamisi ili kuweza kuondoa tatizo hilo la majeruhi.
Taarifa kutoka kwenye mtandao rasmi wa Bayern inasomeka: “Vipimo alivyofanyiwa siku ya jumatatu, vimeonyesha kwamba Ribery amepata majeruhi ya uvimbe, ambayo baada ya kufanyiwa upasuaji siku ya Alhamisi umeondolewa wote.
“Baada ya kupona jeraha hilo, Ribery ataanza mazoezi mepesi na wiki moja baadae atarudi kwenye mazoezi ya timu.
“Hili linamaanisha atakosa mechi kadhaa ijayo ya klabu ukiwemo mchezo dhidi ya Arsenal katika hatua ya 16 bora ya UCL.”
No comments