Recent comments

Breaking News

Matokeo ya UEFA:- Arsenal yakubali kipigo cha bao 2 kwa sifuri nyumbani, huku AC MIllan pia ikifungwa goli moja uwanja wa nyumbani. Tazama Magoli

Mambo yamekuwa magumu leo huko Italia kwa AC MILAN na Uingereza kwa washika bunduki ARSENAL baada ya kufungwa mabao mawili kwa sifuri katika uwanja wa nyumbani. Dakika za mwanzo Arsenal ndio ilikuwa ya kwanza kupata penati kupitia kwa mchezaji wao Ozil lakini hatimaye alikosa Penati hiyo baada ya goli kipa wa Bayern kuicheza vyema pamoja na kupotezwa mwelekeo, dakika chache baadae kabla ya Half-Time Bayern nayo ilipata Penati ambapo Alba alikosa penati kwa kupiga nje.

Matokeo yalisomeka bila bila mpaka kipindi cha pili ambapo kila timu ilimpania mwenzake huku Arsenal ikiwa inacheza pungufu ndani, Krose alipokea safu pasi toka kwa Rooben na hatimaye kutengeneza goli la kwanza kwa Bayern baadae Super Sub Muller alipiga goli safi na kuihakikishia ushindi timu yake Ugenini.


No comments