Diamond kuhudhuria tuzo za 'AFRIMMA' zitakazofanyika Texas Marekani, zitahusisha wasanii wakubwa Afrika
July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards’, na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.
Diamond amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno yanayosomeka, “Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014 Texas, Dallas (USA).”
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine, zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj’s, watayarishaji wa muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika.
Tuzo hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet Ibrahim.
No comments