Chris Brown adai meneja wake wa zamani amevujisha nyimbo kwenye albam yake, meneja nae amjibu
Siku kadhaa baada ya kumaliza muda wa siku 90 alioamriwa na
mahakama kukaa Rehab kwa ajili ya matibabu ya kudhibiti hasira, Chris
Brown amemtuhumu meneja wake wa zamani, Tina Davis kuwa amevujisha
nyimbo za kwenye albam yake ijayo aliyoipa jina la ‘X’.
Katika ujumbe alioundika katika akaunti yake ya Twitter Jumapili
iliyopita, Chris alimtuhumu meneja huyo pia kuwa amekatalia ‘hard drive’
yake ambayo ina nyimbo za kwenye albam yake.
“My old manager is leaking my NEW album music and refuses to give me
my back up hard drive to sabotage my album. That’s F’d up G!” alitweet
Chris Brown na kisha kuifuta tweet hiyo muda mfupi baadae na kuandika,
“Snakes in the grass…..Just stay positive.”
Baada ya kuandika tweet hiyo, meneja huyo wa zamani ambaye amefanya
kazi na Chris tangu mwaka 2005 wakati Chris ana miaka 16, alimjibu
akimtaka afikirie ni wapi ilipoanzia na kwamba atume tuhuma hizo kwa mtu
sahihi aliyefanya.
“@Chrisbrown Trace it! Find out where it originated from…RCA can do
that for you. Then send a defaming tweet out on who really did it.”
Albam ya Chris Brown ‘X’, imepangwa kutoka May 5, mwaka huu.
No comments