Exclusive: Lady Jay Dee aeleza sababu za kujifunza Karate, anataka kumkabili nani? Msikilize hapa
Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na
habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa
Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo
huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.
Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama
Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani
hasa? Haya ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza.
Moko Biashara aka One B wa 100.5 Times Fm alimtafuta Lady Jay Dee na kutuwakilisha kwa kumuuliza maswali hayo nae akafunguka.
“Kwa sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya
kitu saa zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya.
Kwa hiyo nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka
Anaconda.
Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote.
“Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili
ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo
likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.
Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii.
“Ni mwanzo tu lakini mimi mwenyewe ni mwanafunzi mwenye bidii, bidii
yako pale ndio itakayokufanya uweze ku-improve kwa muda mfupi.” Lady Jay
Dee alimwambia Moko Biashara aka One B.
Msikilize hapa:
No comments