HIVI NDIVO KELVIN YONDANI ALIVYOSAINI NA MENEJIMENTI YA YANGA
Kelvin Patrick Yondani beki wa kati wa Simba amekana kusaini mkataba wowote na Simba na amesema yeye amesaini Yanga tu mkataba wa miaka miwili, ameongeza kwamba Simba wanampakazia kusaini mkataba mpya na anataka wapenzi wote wa soka Tanzania watambue kwamba kuanzia sasa yeye ni mchezaji halali wa Yanga.
“Kesho tutaongea vizuri, nimechoka,”alisema Yondan baada ya kukamilisha usajili wake, mbele ya mgombea Ujumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb.
Bin Kleb amesema “Alikuwa amesaini kila kitu, kuna sehemu alikuwa hajamaliza kujaza leo, ndio amemalizia na ametuhakikishia hana mkataba na Simba, hivyo huyu ni mchezaji ambaye mimi na Seif tunamsajili kwa ajili ya klabu yetu kipenzi, Yanga,”
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata ni kwamba, Yondan aliikana Yanga awali kwa sababu walimsainisha fomu bila kumpa fedha, lakini leo amepewa Milioni 30 zake taslimu na amemaliza kila kitu. (Stori imeandikwa na bongostaz.blogspot.com )

No comments