ALICHOSEMA TEVES KUHUSU KURUDI KWAO
Staa wa soka kutoka Argentina ambae alizinguana na kocha wa club yake ya Man City msimu uliopita Carlos Tevez amerudi kwao Argentina na kuongea kwenye event iliyoandaliwa na club yake ya zamani ya Boca Juniors kwamba anafurahia kuichezea Man City lakini angependa kumalizia soka lake kwenye club hiyo ya Boca Juniors.
Amesema anatamani maisha yake ya soka ayamalizie akiwa na jezi ya Boca Juniors na aliwahi kufikiria hivyo hata wakati anaiacha club hiyo, Teves aliichezea Boca juniors kuanzia 2001 – 2004 na aliifungia magoli 26, ameichezea Man City kuanzia 2009 mpaka sasa na ameifungia magoli 48.
Hata hivyo Teves amesema hana haraka ya kuondoka Man City na ikitokea nafasi ya yeye kuondoka angependa kwenda kumalizia soka lake Boca Juniors.
No comments