Recent comments

Breaking News

MBUNGE AKIANGALIA PICHA ZA NGONO BUNGENI!



hivi ndio ilivyokua, waziri wa kulia kanogewa mpaka kapanua miguu.
Kwa aibu kubwa sana, Waziri mmoja wa India ambae pia ni mbunge amekutwa akiangalia picha za ngono kwenye bunge la nchi hiyo wakati vikao vya bunge vikiendelea kama kawaida ambapo waziri huyo alikua busy kwenye simu akiangalia picha hizo.
Hiyo ishu ilionekana kwenye tv baada ya cameraman aliekua juu, kuvuta picha ya waziri huyo wa ushirikiano bwana Savadi na hivyo kuonesha kila kitu alichokua anafanya mbunge huyo ambapo cha kusikitisha zaidi picha hizo hizo zilionyesha waziri mwenzake wa mazingira akichungulia kwenye simu ya mwenzake na baadae kutabasamu.
Kwa kujitetea mawaziri hao waliitisha kikao cha dharura na waandishi wa habari huku wakisema walikua wakitazama mwanamke mmoja akiwa anabakwa kwenye movie moja ya kizungu, na sio kweli kwamba walikua wanatazama picha za ngono.
Cameraman mmoja anaedai kupiga picha hizo amesema yeye na cameraman mwenzake dakika 15 kabla ya bunge kuisha, walishuku kwamba kuna ishu baada ya waziri huyo kuonekana akiwa ameficha simu katikati ya miguu yake huku mwenzake akichungulia, na walivotua picha hizo kwa karibu ndio wakakuta ni picha za ngono.
Wakati hayo yote yanatokea bungeni, bunge lilikua linajadili ishu muhimu ya ukame ambapo spika wa bunge japo hajaziona picha hizo, amesema wawili hao watachukuliwa hatua kali kama hiyo stori ni ya kweli.
Picha ya pili hapo juu ni baadhi ya watu waliokamatwa na polisi baada ya kuandamana mpaka nyumbani kwa mmoja kati ya mawaziri hao wakitaka ajiuzulu, hapo wanapakizwa kwenye karandinga la polisi.

No comments