
.

Baada ya kumpiga rais wa nchi hiyo, wananchi wakawa wamepumzika hapo hapo Ikulu.

.
Hizi picha ni wakati
waandamanaji wenye hasira walipovamia na kumpiga Rais wa muda wa Mali
Diancounda Traore juzi ambapo ilikua kama mzaha, waandamanaji hao
waliokua na hasira walivamia Ikulu ya nchi hiyo na kumpa kipigo rais
huyo huku walinzi wake wakitizama, hasira za raia hao zilisababishwa na
kitendo cha Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magahribi, ECOWAS
kumlaazimisha kiongozi wa mapinduzi ya Machi 22 Kapteni Amadou Sanogo
akubali kuongeza muda wa serikali ya mpito inyoongozwa na rais Traore
kwa miezi kumi na mbili.
Msemaji wa wanajeshi
waliyofanya mapinduzi hayo Bakary Mariko, alisema walinzi wa rais Traore
waliua watu watatu katika uvamizi huo japo taarifa nyingine zinasema
walinzi hao walikaa na kutizimana huku wananchi hao wakijivinjari katika
viwanja vya Ikulu, huku wengine wakionekana kuegesha pikipiki na
baiskeli zao katika eneo la ikulu na kuchana picha za rais Traore.
No comments