NYIMBO MBILI ZILIZOMPA MARLAW MAFANIKIO ZAIDI TOKA APIGWE MUHURI KWENYE BONGO FLEVA.
Amesema “wimbo wa Bembeleza ambao ndio ulikua wa kwanza uliopelekwa redioni bila mimi kufahamu kwa sababu nilirekodi kimasihara, ndio wimbo ambao umenipa tuzo, umenivuta kufanya muziki kitu ambacho nilikua naota, heshima na kunitangaza sana kulikonipa tuzo mbili za KTMA, Wimbo bora wa mwaka na mwimbaji bora wa kiume.
Wimbo mwingine ni Pipi ambao uliniletea tuzo nne, Kenya mbili na KTMA 1 na nomination ya Nigeria Sound City Tv, pia hii single iliniletea pesa na kunifanya nifannye vitu ambavyo nilikua naviwazia kwenye ndoto ikiwemo kununua gari la ndoto yangu ambalo ni Mercedes Benz ML la milioni 25.
Baada ya miezi sita kupita toka aachie single mpya mwaka jana, Marlow ametoa wimbo wake mpya May 25 2012 unaitwa Kirungu ukiwa ni wimbo ambao hauzungumzii mapenzi, anamzungumzia mtoto mtukutu.
No comments