KOCHA MILOVAN WA SIMBA AONGEZEWA MKATABA, STORI KAMILI NDIO HII!

KLABU ya Simba ya Dar es
Salaam imemuongezea mkataba wa miaka miwili kocha wake Mserbia, Profesa
Milovan Cirkovic baada ya kuridhishwa na kazi yake kwa kipindi cha nusu
msimu alichokuwa na timu hiyo tangu arithi mikoba ya Mganda, Moses
Basena.
Mwandishi Bin Zubery wa
bongostaz.blogspot.com ameandika kwamba Makamu Mwenyekiti wa Simba SC,
Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba Milovan atakuwa kocha wa Simba
kwa miaka miwili zaidi tangu sasa baada ya kuongezewa mkataba.
“Kipimo cha mafanikio ya
kocha ni mataji na soka safi, kitu ambacho sisi kama viongozi
tumekishuhudia Simba chini ya Profesa Milovan, sasa hatuoni kwa nini
tusimuongeze mkataba,”alisema Kaburu.
Pamoja na kuipa ubingwa wa Ligi
Kuu ya Bara kwa kishindo, Milovan aliiwezesha Simba kufika hatua ya 16
Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako ilitolewa kwa penalti 9-8 na
Al Ahly Shandy ya Sudan, baada ya sare ya jumla ya 3-3.
No comments