Recent comments

Breaking News

SABABU YA GOOGLE ADSENSE KUZIKATALIA(KUTOAPPROVE) BAADHI YA WEBSITES NA BLOGS..

Kama wewe ni mmiliki wa blog au website na mara kadhaa umejaribu kuunganisha blog yako na
mfumo wa matangazo wa google adsense na kukataliwa kila unapojaribu kufanya hivyo.Google adsense kama kampuni yoyote kubwa wana policy,terms,conditions na masharti mengine na haitokuwa kazi rahisi kukubaliwa na google adsense ikiwa publisher au blogger atakuwa yupo kinyume na hayo masharti.
Turudi kwenye mada kuu, “kwanini google adsense wanadisapprove baadhi ya blogs” fuata mtiririko hapo chini…

Lugha
Mpaka sasa google adsense wanasupport blogs ambazo zipo katika lugha zifuatazo ,Arabic,Bulgarian,Chinese(simplified),Chinese(traditional),Croatian,Czech,Danish,Dutch,English,Estonian,Finnish,French,German,Greek,Hebrew,Hungarian,Indonesian,Italian,Japanese,Korean,Latvian,Lithuanian,Polish,Norwegian,Portuguese,Romanian,Russian,Serbian,Slovak,Slovenian,Spanish,Swedish,Thai,Turkish,Ukranian,Vietnamese kama blog yako haipo katika hizo lugha itakuwa ngumu kwa blog yako kuwa approved na google adsense.

Yaliyomo ndani ya blog au website yako
Google adsense hawazikubali blog zinazoonyesha vitendo vya ngono na utupu,blog zinazohamasisha vitendo vya uhalifu,unyanyasaji na ubaguzi wa aina yoyote,blog zinazoonesha matukio ya ukatili na unyama(hasa kwa watoto) na vilevile google adsense hawazikubali blog zinazokiuka sheria za hakimiliki.

Watembeleaji wachache
Google adsense haitoikubali blog yenye watembeleaji wachache kwa siku.Inavyosemekana inahitajika kuwa na watembeleaji zaidi ya hamsini kwa siku kuwa approved na google adsense.Usikurupuke kujiunga na google adsense kama hauna watembeleaji wa kutosha.

Muonekano wa blog/website yako
Itakuwa ngumu kwa google adsense kukubali blog zenye mpangilio na muonekano mbovu kwa mfano ugumu wa kusoma maandishi,mpangilio mbovu wa button kiasi cha mtembeleaji kutojua nini la kufanya.

Uchanga wa blog yako
Google adsense inakatalia blog zote ambazo hazijafikisha miezi sita toka kuanzishwa kwake.Tumia huo muda wa miezi sita kuijenga blog yako kabla ya kujiunga na google adsense.

Privacy policy
Privacy policy inasaidia kumuepusha blogger na google kujiingiza kwenye matatizo yanayotokana na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za udhibiti wa taarifa.Kama blog au website yako haina privacy policy itakuwa ngumu kwa adsense kukuapprove.

Mbali na hayo kuna sababu zingine zinazoweza kufanya blog yako isikubaliwe na google adsense kwa mfano kunakili kazi ya blogger mwingine kwenye blog yako(copy&paste) na kuwa na post chache zisizozidi hamsini.

Fanya kazi zako kwa umakini na kiuweledi(professional),kuwa na subira utafanikiwa tu…..


1 comment:

  1. Asante sana kwa elimu hii,Mimi nimejaribu KUOMBA Google AdSense ikakataliwa na website yangu ni

    www.tenachew.com

    Nimejifunza mengi kwa article yako. Asante sana

    ReplyDelete