Recent comments

Breaking News

Kombe La Dunia: Safari ya Brazil, tuangalie kikosi cha wenyeji Brazil mwaka 2014.....

Timu ya taifa ya Brazil ni taifa pekee lililotinga katika fainali za mwaka huu, pasi na kupita kwenye michezo ya kufuzu, kufuatia sheria ya uenyeji ambayo inawabeba na kuingia moja kwa moja katika fainali hizo ambazo zitachezwa katika miji 12 nchini humo.
Hata hivyo kijografia nchi hii ipo katika ukanda wa Amerika ya kusini na kama ingeanzia hatua ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia ingecheza michezo yake katika ukanda huo na timu nyingine kama Chile, Venezuela, Bolivia, Colombia, Argentina, Peru, Paraguay, Uruguay pamoja na Ecuador
Viwango vya ubora wa soka duniani: 4
Katika historia ya ushiriki wa fainali za kombe la dunia.
Brazil ndio nchi pekee iliyotwaa ubingwa wa dunia mara nyingi, kuliko nchi yoyote duniani iliyoshiriki fainali za kombe la dunia tangu mwaka 1930, ambapo fainali za kwanza zilichezwa nchini Uruguay.
Brazil wametwaa ubingwa wa kombe la dunia mara tano katika fainali za mwaka 1958 (Sweden), 1962 (Chile), 1970 (Mexico), 1994 (USA) pamoja na 2002 (Korea kusini na Japan).
Taifa la Brazil limeshiriki fainali za kombe la dunia mara 18, na kwa mwaka huu itakua ni mara ya 19.
Fainali za kombe la dunia ambazo zilishuhudia Brazil wakishiriki ni zile za mwaka 1930 nchini Uruguay, 1934 (Italia) , 1938 (Ufaransa), 1950 (Brazil), 1954 (Uswiz), 1958 (Sweden) ,1962 (Chile), 1966 (Uingereza), 1970 (Mexico), 1974 (Ujerumani Magharibi), 1978 (Argentina), 1982(Hispania), 1986 (Mexico) ,1990 (Italy), 1994 (USA) ,1998 (France), 2002 (Korea kusini & Japan), 2006 (Ujerumani) pamoja na 2010(Afrika kusini)
Kufuatia ushiriki huo wa timu ya taifa ya Brazil, taifa hili la Brazil linakuwa moja ya mataifa yaliyoshiriki katika fainali zote za kombe la dunia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930 kule nchini Uruguay.
Wachezaji Muhimu

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Neymar da Silva Santos Júnior, ni sehemu ya wachezaji wanaotarajiwa na maelfu ya mashabiki duniani kote katika harakati za kuonyesha kiwango kizuri katika fainali za mwaka huu.
Wengine ni Dani Alves, Hulk, Ramires, Fred, Paulinho pamoja na Julio Cesar.
Kocha: Luiz Felipe Scolari (Mzawa)
Jina la timu ya taifa ya Brazil: Canarinho (Little Canary)
Wachezaji waliowahi kutamba wakiwa na timu ya taifa ya Brazil miaka ya nyuma: Manuel Francisco dos Santos Garrincha, Edson Arantes do Nascimento Pele, Ronaldo Luís Nazário de Lima Ronaldo, Romário de Souza Faria, José Roberto Gama de Oliveira Bebeto pamoja na Arthur Antunes Coimbra Zico
Katika fainali za kombe la dunia za mwaka huu huko nchini Brazil timu ya taifa ya Brazil imepangwa katika kundi la kwanza sambamba na timu ya taifa ya Croatia, Cameroon pamoja na Mexico.
Timu ya taifa ya Brazil itaanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa kombe la dunia
Arena de São Paulo, São Paulo
12 June 2014
Brazil          Match 1       Croatia
                 
Estádio Castelão, Fortaleza
17 June 2014
Brazil          Match 17     Mexico
23 June 2014

Estádio Nacional Mané Garrincha, Brasília
Cameroon           Match 33     Brazil

No comments