Filamu ya Zena na Betina kughairishwa kutoka kesho Mei 29.....Unajua kwanini.....?Isome hapa
Muigizaji wa filamu hapa Tzee Salma Jabu Nisha ametoa taarifa za kugailisha filamu yake mpya ya ‘Zena Na Betina’ ambayo ilitakiwa kutoka kesho 29 Mai,kupitia acont yake ya facebook alisema.
“Habari mashabiki zangu, nyumbani kwetu akifa baba au dada au mwanafamilia yeyote, basi kama kuna aliyetaka kuolewa harusi inaghairishwa. Maisha yangu ni filamu, na filamu ni nyumba yangu ya pili, sisi kama Nisha’s Film Production na Steps Intertainment tumeamua kughairisha kuitoa filamu yetu mlokuwa mkiisubiri kwa hamu ‘Zena Na Betina’, ilikuwa itoke tar.29/05/2014 sasa basi tutaisogeza mbele hadi tar.12/06/14 kwa ajili ya kuomboleza misiba hii.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza,munisamehe sana,tumeguswa sana,kwangu mimi kama Nisha kutoa filamu ni furaha,siwezi kufurahi siku tunayomzika msanii mwenzetu kipenzi Rachel yaani kesho ambayo ndio ilikuwa siku ya kutoka Zena na Betina . Hii ni zawadi yenu Rachel na Adam kuambiana,kutoka Nisaha’s Film Production, nimetazama utu kwanza halafu pesa baadae.
wanaoendelea kufanya promo wafanye na naomba mnisaidie kusambaza ujumbe huu. Nawapenda sana”.
No comments