Oscars 2014: Lupita Nyong'o apata tuzo ya 'Muigizaji bora wa kike msaidizi', 12 Years A Slave yabeba tuzo 3 (Orodha kamili)
Maombi ya raia wengi wa Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla yamesikika. Muigizaji wa kike wa Kenya Lupita Nyong’o ameng’ara katika tuzo kubwa duniani, tuzo za Oscar baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele cha muigizaji bora msaidizi wa kike.
Tuzo hizo zilizofanyika Jumapili, March 2,2014 zilifuatiliwa kwa ukaribu na vyombo vyote vikubwa vya habari duniani huku zikioneshwa pia kupitia mtandao wa ABC.
Baada ya kupokea tuzo hiyo, Lupita Nyong’o alitoa heshima zake kwa Patsey, mtumwa wa miaka ya 1840 ambaye aliigiza nafasi yake kwenye 12 Years A Slave.
“I doesn’t escape me for one moment that so much joy in my life is because of so much pain in someone else’s.” Alisema Lupita.
Filamu ya 12 Years A Slave ilishinda tuzo tatu, ukiacha hiyo alishinda Lupita Nyong’o nyingine ni ‘Best Picture’ na nyingine ni ‘Best Adapted Screenply’ aliyopewa John Ridley.
Brad Pitt ambaye ni moja kati ya watayarishaji wa 12 Years A Slave, aliipokea tuzo ya Best Picture na kumpa muongozaji wa filamu hiyo McQueen.
“Everyone deserves not just to survive, but to live.” Alisema McQueen.
Katika tuzo hizo, filamu ya ‘Gravity’ ilizifunika filamu zote kwa kuondoka na tuzo saba ikiwa ni pamoja na tuzo aliyopewa muongozaji wa filamu hiyo Alfonso Cuaron.
Muongozaji wa filamu ya Gravity ambaye ni raia wa Mexico, Alfonso Cuaron alitumia miaka minne kuhakikisha filamu hiyo inakuwa kama ilivyokusudiwa hususani katika masuala ya kiufundi.
Filamu hiyo ilishinda katika vipengele vya Original Score, Visual Effects, sound mixing, sound editing, cinematography na film editing.
Hii ni orodha nzima ya washindi wa tuzo hizo:
-Best Picture: "12 Years a Slave"
-Best Director: Alfonso Cuaron - "Gravity"
-Best Actor: Matthew McConaughey - "Dallas Buyers Club"
-Best Actress: Cate Blanchett - "Blue Jasmine"
-Best Supporting Actor: Jared Leto - "Dallas Buyers Club"
-Best Supporting Actress: Lupita Nyong'o - "12 Years a Slave"
- Best Original Screenplay: Spike Jonze - "Her"
- Best Adapted Screenplay: John Ridley - "12 Years a Slave"
-Best Animated Feature Film: "Frozen (2013)"
-Best Foreign Language Film: "The Great Beauty"
-Best Documentary - Feature: "Twenty Feet From Stardom"
-Best Documentary - Short Subject: "The Lady in Number 6: Music Saved My Life"
-Best Live Action Short Film: "Helium"
-Best Animated Short Film: "Mr Hublot"
Best Original Score: "Gravity" - Steven Price
-Best Original Song: "Let It Go" from "Frozen (2013)" - Kristen Anderson-Lopez and Robert Lopez
-Best Sound Editing: "Gravity" - Glenn Freemantle
Best Sound Mixing: "Gravity" - Skip Lievsay, Niv Adiri, Christopher Benstead, and Chris Munro
- Best Production Design: "The Great Gatsby" - Catherine Martin (Production Design); Beverley Dunn (Set Decoration)
-Best Cinematography: "Gravity" - Emmanuel Lubezki
-Best Makeup and Hairstyling: "Dallas Buyers Club" - Adruitha Lee and Robin Mathews
-Best Costume Design: "The Great Gatsby" - Catherine Martin
-Best Film Editing: "Gravity" - Alfonso Cuaron and Mark Sanger
-Best Visual Effects: "Gravity" - Tim Webber, Chris Lawrence, Dave Shirk, and Neil Corbould
No comments