Jokate aeleza kinachomvutia zaidi kwa Lupita Nyong'o, adai weledi ni kitu alichojifunza kutoka kwake.
Jokate Mwegelo amemzungumzia muigizaji wa kike raia wa Kenya, Lupita Nyong’o aliyegeuka mada kubwa Marekani na kung’aa katikati ya mastaa wa Hollywood baada ya kushiriki katika filamu ya 12 Years a Slave.
Akiongea na mtandao wa Bongo5, Jokate Kidoti amesema alivutiwa sana na uigizaji wa Lupita Nyong’o kwenye filamu ya 12 Years A Slave na kwamba kuna vitu ambavyo vinamfanya amkubali zaidi ikiwa ni pamoja na jinsi anavyoitumia ngozi yake nzuri.
Ameeleza pia jinsi ambavyo Lupita ameweza kukubalika sio tu kwa watu wa kawaida lakini pia kwa wataalam na wahusika wazuri katika tasnia husika.
“There is one thing Wananchi kukupenda, and there is another thing watu ambao wanajua the craft, wanaoujua ugumu wa ile kazi, ubora, good actor/actress kukuapreciate. So far she has that kind of support like her peers appreciate her. Napenda anavyotumia ngozi yake. Her skin is very nice. At the same time she very daring. Nimeona vitu amevaa kama Victoria Beckham, Victoria Beckham pia akampost kwamba she was wearing one of her clothes and she is not afraid of and really love that about her.” Amesema Jokate.
Kitu kikubwa ambacho Jokate anajifunza kutoka kwa Lupita Nyong’o ni jinsi anavyofanya kazi zake kwa kuzingatia weledi, kwa kuwa Lupita amesomea vitu anavyovifanya.
“Lupita amepita training mbalimbali, it makes you understand your craft.” Amesema Jokate.
“Na vile vile kutokata tamaa. She is 30 years old, her first role, her first Oscars nomination wakati kuna watu wengi wanafanya movies nyingi lakini hawafikii level aliyoifikia yeye. Hakuna kukata tamaa, always thing positive, penda kujifunza.”
Chanzo: Bongo5
No comments