Katy Perry aondoa kipande kilichodaiwa kumkufuru Mungu kwenye video yake 'Dark Horse'
Hatimaye Katy Perry anadaiwa kusalimu amri baada ya jamii ya Kiislamu ya Uingereza kuitaka YouTube iiondoe kabisa video yake ‘Dark Horse’ kwa madai kuwa ilikuwa inakipande kinachomdhalilisha au kumkufuru Mungu na kumuonesha kuwa ameshindwa na nguvu za giza.
Kwa mujibu wa Shazad Iqbal ambaye alianzisha kampeni ya kutaka video hiyo iondolewe na akakusanya sahihi zaidi ya 65,000, video hiyo imehaririwa na kuondoa kipande kilichokuwa kinamuonesha mwanaume aliyevaa cheni iliyoandikwa ‘Allah’, mwanaume aliyeishia kuchomwa moto na kuuawa baada ya kuzidiwa na nguvu za giza.
“Guys ninayofurah kuwataarifu kuwa jina la ‘Allah’ limeondolewa kwenye video ya ‘Dark Horse’. Tusingeweza kufanya hivyo bila sapoti ya kila mmoja, kwa hiyo namshukuru kila mmoja sauti yetu imesikika. Mungu awabariki wote.” Amesema kupitia Shazad.
Wiki iliyopita, jamii ya kiislamu ya Uingereza ilipinga vikali na kulaani kitendo kilichokuwa kikioneshwa na Katy Perry kwenye video hiyo, na kisha kuanzisha ‘petition’ iliyokusanya kura za watu wanaotaka video hiyo iondelewe YouTube.
‘Dark Horse’ ni wimbo wa Katy Perry aliomshirkisha Juice J na umeshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard 100 kwa wiki nne mfululizo, na upo kwenye albam yake ya ‘Prism’
No comments