Recent comments

Breaking News

Aunt Ezekiel aeleza kilichomsukuma kufanya Bongo Flava, auelezea wimbo wake 'Mguu kwa Mguu' aliofanya na Linex

Aunt Ezekiel aeleza kilichomsukuma kufanya Bongo Flava, auelezea wimbo wake
Msanii wa filamu za Kiswahili, Aunt Ezekiel ambaye anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa Bongo Flava alioupa jina la ‘Mguu kwa Mguu’ aliomshirikisha Linex Mjeda, ameeleza sababu kubwa iliyomfanya aingie kwenye game la Bongo Flava.
“Unajua game la Tanzania linabadilika badilika kwa hiyo nimeona ngoja pia nijihusishe katika uimbaji ili niendelee kuteka mashabiki, mimi zamani nilikuwa napenda sana Bongo Flava na sio kwamba nilikuwa naimba hapana, nilikuwa kama nikiona wasanii wakianza kuimba basi moyoni nafurahi sana. Siku moja wakanipa ushauri na hapo ndipo nikaingia studio na kutengeneza wimbo wa ‘Mguu kwa Mguu.” Aunt Ezekiel ameiambia tovuti ya Times Fm.
Ameeleza kuwa alitegemea kuachia wimbo huo mwaka jana ila ratiba zake hazikwenda vizuri hivyo aliamua kuiachia rasmi mwaka huu.
Mguu kwa Mguu ni wimbo uliotayarishwa na Mr. T Touch ndani ya Seductive Records 

No comments