Exclusive:- Msikize P The MC akikosoa wimbo wa Roma 'KKK', adai amerap kiuoga, "anapigana na anaemuogopa"
Wimbo wa Roma KKK (Karibu Kwenye Karamu) haukumuingia akilini ‘positively’ rapper wa Tamaduni Music na ngome ya Miraba Minne, P The MC ambaye amedai kuwa Roma aliyekuwa anamfahamu yeye sio Roma aliyemsikia kwenye wimbo huo.
Wiki iliyopita, baada ya kuachiwa rasmi ‘KKK’, P The MC aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma ana Stress, japo hakutoa maelezo hadi aliposikikia kupitia The Jump Off ya Times Fm inayoendeshwa na Jabir Saleh aka Kuvichaka.
“Nimebahatisha kusikia wimbo wa Roma unaitwa KKK, nimebahatika kuusikiliza leo kuna mtu alikuwa nao nikamuomba anipe niusikilize vizuri. Nilipomsikiliza nikagundua kuwa Roma ninayemfahamu mimi na Roma aliyefanya kwenye wimbo ule ni Roma wawili tofauti. Kwa hiyo kuna kitu ambacho kimetokea ndicho kimemfanya a-act hivyo, yaani afanye ule wimbo.” P The MC aliiambia The Jump Off ya 100.5 Times Fm.
“Hakuna ubaya kufanya ule wimbo wa aina ile ambao umeongelea watu wengi wa aina tofauti, lakini lengo limeonekana kabisa ulikuwa ni straight kwa mtu mmoja, hilo ndilo tatizo. Nakumbuka wakati wanatoka vinega sijui anti-virus kila mtu alikuwa anajua lengo la wale jamaa kuwa wameelekea upande gani. Lakini huyu jamaa niliposikiliza nikagundua lengo lilikuwa straight kwenda kule. Ila cha ajabu humo ndani akaanza kuwagusa watu wengine ambao hawahusiki upande ule wala upande huu.” Aliongeza rapper huyo wa Tamaduni.
“Kwa hiyo ule unaitwa ni uoga. Yaani wewe unapigana na unaemuogopa, ni tatizo hilo. Kwa hiyo mimi sikupendezewa na hicho kitu ndio maana nikaandika huyu jamaa ana stress.”
P The MC aliguswa na mstari wa Roma unamtaja Songa kwa mshangao kuwa hata Lady Jay Dee anamfahamu.
“Jide kumjua Songa sio kitu cha kushangaza kwa sababu Jide kamjua Roma ambaye akina Songa hapa wanaanza kuchana na akina Roma wanaanza kuchana nafikiri ni miaka hiyo hiyo. Roma sio legendary kusema alianza na akina Profesa au vipi. Jide kama alimjua Roma aliyekuja juzi kwenye muziki basi sio ajabu akimjua Songa pia hakuna tatizo.
“Kwa hiyo huo mstari unaonesha kabisa wewe jamaa ulikuwa na stress zako binafsi zimekuumiza kichwa kwa muda mrefu, ukakaa chini ukashika karatasi ukasema kabisa naandika eti mpaka Jide kamjua Songa, mbona kakujua wewe hatu hatujashangaa?”
Msikilize hapa kwa urefu zaidi:
No comments