Exclusive: Diamond Platinumz na Queen Darleen=? Read it more
Unaweza kukosa jibu la haraka haraka ukiulizwa swali hilo lakini pengine jibu la swali na kiu ya mashabiki wa muziki itakatwa baada ya kukamilika kwa kazi itakayowaunganisha ndugu hao wa damu ambapo kwa sasa wameanza kusambaza picha mbalimbali kwenye akaunti zao.
Ukiingia kwa sasa kwenye akaunti za Diamond Platnumz na Queen Darleen utaziona picha hizi ingawa bado hawajaweka wazi nini kinafuata lakini kwa picha hizi zinaonyesha ujio wa collabo ya ndugu hawa wawili wa damu wanaotoka kiwanda kimoja cha Bongo Fleva.
Endapo watafanikiwa kutoa wimbo wa pamoja ukitoa zile zinazowaunganisha kama Kigoma All Stars,hii inaweza kuwa kwenye orodha ya collabo zilizofanywa na ndugu wa damu,kama Joh Makini na Nick wa Pili,Maunda Zoro na Banana Zoro,Ally Kiba na Abdul Kiba,Dataz na Squeezer na za ndugu wengine.
No comments