Recent comments

Breaking News

Black Rhino asema wimbo aliofanya na Ngwair 'Lookie Lookie' ni baraka, hakumuona tena baada ya kuikuta sauti yake kwenye wimbo huo

Black Rhino asema wimbo aliofanya na Ngwair
Member wa Choka Mbaya, Black Rhyno ambaye anatarajia kuachia wimbo wake mpya mwezi huu aliomshirikisha marehemu Albert Mangwea aka Ngwair ‘Lookie Lookie’ hauchukulii wimbo huo kama hit song ijayo tu, bali ni baraka pia.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, rapper huyo ameelezea jinsi ambavyo wimbo huo ulivyofanyika na kudai kuwa alikuwa na ahadi ya kufanya wimbo mmoja na Ngwair japo hawakupanga uwe wimbo huo aliokuwa ameanza kuurekodi.
“Ngoma ya mimi na Albert ilikuwa ifanyike siku nyingi sana na kila siku tulikuwa tukionana tunataniana hivyo ‘ebana ngoma yetu tunadaiana unajua’. Lakini kila siku ilikuwa haifanyiki kwa kuwa kila mtu alikuwa na misele yake mingi mingi, huyu anaenda huku anapiga issue yake hivi anapiga issue yake vile.” Amesema Black Rhyno.
“Kwa hiyo ilivyotokea wakati mimi nafanya hii ngoma…actually mimi naichukulia kama blessing au naweza kusema tulikuwa tuna kitu mioyo yetu ilikuwa inatakiwa kufanya kwa pamoja.”Ameongeza.
Black Rhino ameeleza kuwa wakati yuko studio kwa producer Mbezi anarekodi, Ngwair alimwambia kuwa huo wimbo ameupenda kwa hiyo anaweza kufanya chochote japo hakusema ataingiza verse yake.
“Mimi nikawa nimefanya session yangu nimeondoka. Siku nyingine kabisa nimeenda studio ndio Mbezi anakuja ananisikilizisha ananiambia ‘ebana eeh...unajua Albert ngoma yako alii-mind sana na akasema haiwezekani akaiacha hivi hivi kwa hiyo aliandikia verse na akarekodi the same night wakati wewe umeondoka’, na ngoma ikawa imefanyika hivyo.” Amesimulia rapper huyo wa Choka Mbaya.
“By the time anafanya yeye ndio anaenda kufariki, kwa hiyo yaani mimi kwangu naichukulia kama blessing. Halafu nimerudi studio nakuta kwamba amenifanyia verse halafu yeye ameondoka, na ndivyo alivyoondoka hakurudi tena Mangwea.”

No comments