Arjen Robben ahatarisha ndoa ya Pep Guardiola
Siku moja baada ya mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Arjen Robben, kukamilisha dili la kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa soka barani Ulaya pamoja na nchini Ujerumani FC Bayern Munich meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola, ametoa lililo moyoni mwake kuhusu namna ya mshambuliaji huyo anavyoharibu maelewano kati yake na mkewe Cristina.
Pep Guardiola, amesema pamoja na kufurahishwa na hatua ya Arjen Robben kukubali kusiani mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya mjini Munich, bado ana wasi wasi na uhusiano na mkewe kutokana na mshambulaiji huyo kuwa shabiki mkubwa wa Cristina.
Guardiola, amesema mara kadhaa amekua akipata wakati mgumu wa kumsikiliza mkewe, kutokana na hitaji la mtu huyo ambae ni muhimu katika maisha yake la kutaka kumuona Arjen Roben akicheza kila siku.
Guardiola, amabe aliwahi kukinoa kikosi cha FC Barcelona kwa mafanikio makubwa amesema, mkewe Cristina siku zote anapenda kumuona Arjen Robben akiwa uwanjani pale FC Bayern Munich inapocheza, na anapokaa nje humsumbua kwa kumuuliza kwa nini mchezaji huyo hachezi.
Guardiola, amesema amekua akitumia muda wake umuelewesha mkewe namna soka linavyochezwa kupitia mifumo mbali mbali ambapo baadhi ya mifumo hiyo haitowi nafasi kwa Robben kucheza, lakini bado maswali kutoka kwa Cristina hujirudia kwa kuhisi huenda wakati mwingine anashindwa kumtumia mshambuliaji huyo kwa kigezo cha kumchukia.
Hata hivyo Pep Guardiola, amesema anaamini mkewe ni shabiki mkubwa wa Arjen Robben, lakini katu hawezi kufanya kazi ya kumfurahisha mke wake kwa kutaka matakwa yake yatimie ya kumuona mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akicheza kila mwishoni mwa juma, na badala yake amekua akitumia ujuzi na maarifa ya kuwatumia wachezjai wengine.
No comments