Valentine's Day: Beyonce azindua nguo za ndani maalum kwa wapendanao
Wataalam wa misemo ya Kiswahili wanasema ‘ukikaa karibu na Waridi lazima unukie’, hivi ndivyo inavyotokea kwa Beyonce Knowles ambaye ni mke wa mwanamuziki mkubwa na mfanyabiashara anayejua wapi mkwanja upo akautege, bwana Shawn Corey Carter aka Jay Z.
Beyonce ambaye ni mwimbaji, mchezaji mzuri, mtengenezaji wa perfume, muigizaji na bila kusahau kuwa ni mama mzuri wa mtoto wake ‘Blue Ivy’, ametumia fursa ya siku ya wapendanao kuandaa bidhaa ya nguo za ndani maalum kwa wapendao.
Mwimbaji huyo ametoa toleo la nguo za ndani zenye rangi nyeusi ambazo wanawake wanaweza kuwanunulia wapenzi wao kwa $40 huku zikiwa na ujumbe ‘Yours’na nyingine ‘Mine’.
Lakini pia ametoa na sweta ambazo zina maandishi ya majina ya baadhi ya nyimbo zilizoko kwenye album yake aliyoipa jina lake mwenyewe ‘Beyonce’.
No comments