Drake azungumzia uhusiano wake na Rihanna, na kuhusu uhusiano wa mapenzi
Leo ni siku ambayo kama kweli ‘rangi nyekundu’ ndiyo ishara ya upendo basi dunia imekuwa nyekundu kwa jinsi kila mmoja anavyoelezea hisia zake kwa ampendae.
Rapper wa Young Money, Drake nae ameelezea uhusiano wake na mwimbaji wa Caribbean Rihanna aka RiRi ambaye aliwahi kuzungumziwa kuwa sababu ya ugomvi mkubwa kati ya rapper huyo na Chris Brown aliyekuwa mpenzi wake.
Drake ambaye jina lake halisi ni Aubrey Drake Graham, alieleza katika interview aliyofanya na jarida la Rolling Stone kuwa yeye na mwimbaji huyo ni marafiki tu wanaufurahia maisha pamoja.
“She’s the ultimate fantasy. I mean, I think about it. Like ‘Man, that would be good’. We have fun together, she’s cool and s**t. But we’re just friends, she’s my dog for life.” Alisema Drake.
Aliongelea pia kuhusu uhusiano wa mapenzi na mpango wa kuwa na mpenzi, ambapo alidai kuwa hana mpango wa kuwa na mpenzi kwa sasa, na kwamba hana mzuka wa kutafuta mapenzi kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita. Na kwamba bado hajakutana na mtu ambaye anayefanya awaone watu wengine hawana mpango.
“I’m not after p***y like I was three years ago, when I was trying to make up for all the years when no girl would talk to me. But I haven’t met somebody that makes everybody else not matter.”
No comments