Haya ndio maneno ya Nisher kuhusu video ya Nje ya Box, Kijukuu na Baby ya Mirror kuchezwa Channel O
‘Nje ya Box ya Weusi yaoneshwa Channel O’, ni moja kati ya vichwa vya habari vilivyosomeka kwa wingi kwenye mitandao na baadae kuzumgumziwa sana kwenye vituo vya radio na runinga.
Jumatatu ya wiki hii, muongozaji wa video za muziki aliyejipatia umaarufu na mafanikio makubwa kutokana na ubora wa kazi zake, Nisher aliandika Instagram kuonesha kuwa baada ya video ya Nje ya Box ya Weusi kuchezwa Channel O, nyimbo nyingine zinazofuata ni Kijukuu ya Young Dee, Mama Yeyoo ya G Nako na Baby ya Mirror.
Tovuti ya Times Fm iliongea na Nisher na kutaka kufahamu kwa nini nyimbo hizo pekee ndizo zimechagulia, na kama alituma hizo pekee ama alituma nyingi.
“Nilituma kadhaa, na kuna kadhaa hazijapigwa na hizi zilizoenda ndizo zimepitishwa. Nilituma kama sita hivi, sema kuna baadhi zilizopita, ila nyingine wakaeleza kwamba hazitachezwa kwa sababu sio kitu ambacho walikuwa wanakitafuta, au sio kitu ambacho wanakiangalia kukirushwa kwenye station yao.” Amesema Nisher.
Akaweka wazi kuwa aina ya muziki ni kikwanzo kwa baadhi ya video za nyimbo za Tanzania.
“Kwa hiyo zilizopita ndizo zilizokuwa zinakidhi kile wanachokihitaji wao, mojawapo ilikuwa ikiwa ni pamoja na nyimbo..muziki pia, yaani aina ya muziki sio kitu ambacho walikuwa wanakitafuta pia.”
No comments