Exclusive:- Rihanna adai hakupenda kuwa maarufu na alipenda muonekano wa 'jike dume' tangu utotoni
Robyn Rihanna Fenty, Mwimbaji maarufu na mwenye mafanikio makubwa kimuziki na hata katika ulimwengu wa mitindo ameeleza kuwa hakupenda kabisa kuwa maarufu, ila umaarufu ulikuja tu.
RiRi amefunguka wakati akifanya mahojiano na jarida maarufu la Vogue la nchini Marekani, ambapo yeye ndiye atakayelipamba jarada la toleo jipya la jarida hilo litakalotoka rasmi March mwaka huu.
Katika interview aliyofanyiwa na Plum Sykes, mwimbaji huyo alieleza kuwa alikuwa anapenda sana kuimba wakati akiwa mdogo lakini pamoja na kuimba sana hakuwahi kabisa kutaka kuwa maarufu.
“Nilikuwa naimba sana kama mtoto, sana. Nilifanya mazoezi sana kuitengeneza sauti yangu. Napenda kuimba. Nilipenda na haikuwa ratiba ya kila siku. It’s an expression. Sikupenda kuwa maarufu. Nilitaka tu muziki wangu usikike duniani kote. Kisha ikatokea na ikaja na umaarufu.” Rihanna aliliambia jarida la Vogue.
Alifunguka pia kuwa alipokuwa mdogo alipenda sana muonekano wa ki-tomboy aka jike dume, na kwamba alikuwa anapenda sana kuvaa nguo za kiume na kuonekana kama mwanaume.
“Nilipokuwa na umri wa miaka 13 au 14, sikuwa nataka kuvaa nguo ambazo mama yangu alikuwa anataka nivae. Nilikuwa napenda sana muonekano wa kivulana. Marafiki zangu wote walikuwa wavulana. Nilikuwa napenda vitu ambavyo wavulana wanafanya.” Alisema Rihanna.
Aliongeza kuwa kutokana na kupenda muonekano huo, mama yake hakupata shida ya kuchagua nguo kwa ajili yake kwa sababu nguo alizokuwa anamchagulia kaka yake, alichagua kama hizo pia kwa ajili ya Rihanna hivyo wakawa wanavaa saresare.
“Tulikuwa tunavaa jeans zinazofanana, fulana zinazofanana.” Alisema Rihanna na kufafanua kuwa alikuwa anafanya vitu ambavyo viko kinyume na mpangilio wa jamii yake kuanzia maamuzi na muelekeo na kwamba alikuwa anafahamu hicho.
No comments