Recent comments

Breaking News

Exclusive:- Je wajua kuwa siku ya jana ilikuwa ni birthday ya uwanja wa Old Trafford. Fahamu unatimiza miaka mingapi, mjenzi na historia kiufupi

Leo tarehe 19 February 1910 ni miaka 104 kamili tangu uwanja wa klabu bingwa ya Uingereza Manchester United icheze mechi yake ya kwanza kabisa katika uwanja wake wa nyumbani Old Trafford……………………………………………….
Old Trafford ni uwanja wa pili kwa ukubwa ndani ya Uingereza na wa tisa barani ulaya kwa ukubwa, umekuwa ukiboreshwa kila mara tangu ulipobuniwa 1909 na mbunifu wa maarufu wa majengo Archibald Leitch, ambaye pia amehusika na ujenzi wa viwanja kama Anfield – Liverpool, Fulham – Craven Cottage na kiwanja cha Glasgow Rangers – Ibrox Stadium, miongoni mwa vingi.
Ujenzi wa uwanja huo uligharimu kiasi cha £90,000 kwa wakati huo, na mechi ya ufunguzi ilikuwa dhidi ya Liverpool ambapo United walifungwa 4-3. Mechi ilichezwa tarehe kama ya leo miaka 104 iliyopita.
Old Trafford ulichezewa mchezo wa fainali ya FA Cup mnamo mwaka 1911 na pia fainali ya 1915 , mchezo wa kwanza wa kimataifa ulichezwa kwenye uwanja huo miaka 11 baadae.
Uwanja huu ulikumbwa na balaa baada ya kuharibiwa na bomu wakati wa vita vya pili vya dunia, mnamo 8 March 1941, majeshi ya Ujerumani yalipiga mabomu kwenye eneo la Trafford Park Industrial Estate mabomu mawili yakatua kwenye jukwaa kuu la uwanja na sehemu ya kuchezea, jambo lilowalazimu Man United kwenda kugonga hodi kwa mahasimu wao Manchester City waweze kutumia uwanja wao Maine Road kwa kukodisha. Gharama hizo za ukodishaji zilileta deni la karibu £15,000 mpaka wakati Old Trafford ilipofunguliwa mwaka 1949.
Jina la utani la uwanja huo unaoingiza watazamaji zaidi ya 76,000 – Theatre of Dreams lilitolewa na gwiji wa klabu hiyo Sir Bobby Charlton.

No comments