Drake amchana Macklemore kwa kumtumia Kendrick Lamar ujumbe wa kumpoza baada kuwashinda kwenye tuzo za Grammy
Rapper mzawa wa Toronto, Canada, Drake amemchana Ben Haggerty aka Macklemore kwa uamuzi wake wa kuonesha hadharani ujumbe alioumtumia Kendrick Lamar kwa simu baada ya kumshinda kwenye kipengele cha Album Bora ya Rap kwenye tuzo za Grammy mwezi uliopita.
Drake ambaye pia alikuwa akiwania tuzo katika kipengele hicho na album yake ‘Nothing Was The Same’, amefunguka ya moyoni alipokuwa akifanya mahojiano na jarida la Rolling Stone na aliponda kitendo hicho na kumwambia Macklemore kuwa kama alihisi hakustahili basi ajitahidi afanye muziki bora zaidi.
“I was like, ‘You won. Why you posting your text message? Just Chill. Take your W, and if you feel you didn’t deserve it, go get better – make better music.” Alisema Drake.
Mkali huyo wa ‘Started From the Bottom’ alihoji kuwa Macklemore anadhani Kendrick Lamar na wengine waliokuwa kwenye kipengele hicho wangeshinda tuzo hiyo wangemtumia yeye ujumbe?
Hata hivyo, Drake hakuponda kitendo cha Macklemore pekee, aliziponda kiaina tuzo za Grammy na kudai kuwa siku zote katika tuzo hizo huwa hawashindi wasanii bora zaidi katika kiwanda cha muziki.
Lakini alikiri kuwa hata kama Macklemore na Ryan Lewis walishinda tuzo hiyo kwa njia ipi, ukweli ni kwamba waliwavuta watu wengi zaidi yake yeye, Jay Z, Kanye West na Kendrick Lamar.
Katika tuzo za Grammy 2014, Macklemore & Ryan Lewis walishinda tuzo ya album bora ya Rap ya mwaka ‘Best Rap Album’ na album yao ya ‘The Heist’ na kuzishinda ‘Nothing was The Same’ ya Drake, ‘Yeezus’ ya Kanye West, ‘Magna Carta Holy Grail’ ya Jay Z na ‘Good Kid, m.AA.D City’ ya Kendrick Lamar.
Baada ya kushinda tuzo hiyo, Macklemore alimtumia Kendrick Lamar ujumbe mfupi uliosomeka, “You got robbed. I wanted you to win. You should have. It’s weird and sucks that I robbed you. I was gnna say that during the speech. Then the music started playing during my speech, and I froze.”
Baadae aliupiga picha ujumbe huo na kuuweka kwenye Instagram kuwaonesha watu wote na kuandika, “My text to Kendrick after the show. He deserved best rap album.”
No comments