Christina Aguilera kama Lil Kim, atajwa kuwa na ujauzito siku chache baada ya kumtambulisha mpenzi wake.
Mwimbaji Christina Aguilera ameungana na Lil Kim kuwa star anayetarajia kumkaribisha duniani mtoto wake kwa mwaka huu, baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya Matt Rutler siku ya Valentine.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na In Touch Weekly, mama mzazi wa boyfriend wake ‘Matt’ anayejukana kwa jina la Kathleen alifunguka sentensi inayoonesha kuwa mkwe wake anatarajia kupata mtoto pale alipoulizwa ni lini wawili hao watahamia East Coast.
“Sifahamu mipango yao ni ipi, lakini unapokuwa na mtoto huwezi kufikiria kuhusu kwenda sehemu yoyote kwa muda wowote hivi punde.” Alieleza Kathleen.
Hata hivyo, aliongeza kuwa Christina Aguilera na Matt Rutler bado hawajawa na mpango wa kufunga ndoa.
Kama kweli mama Matt ameeleweka vizuri, Christina atampata mtoto wake wa pili kwa kuwa tayari ana mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka sita.
Na anaungana na Lil Kim ambaye anatarajia kupata mtoto na rapper Papers kati ya mwezi June na July mwaka huu.
Us Weekly pia liliripoti kuhusu habari hizo za ujauzito na kuongeza kuwa Christina hatokuwa kwenye dawati la majaji katika msimu wa sita wa shindano la kuimba la ‘The Voice’, na nafasi yake itachukuliwa na Shakira.
No comments