Home
/
Unlabelled
/
Usajili wa dirisha dogo mwezi january itakuwa changamoto kwa timu za Man United, Chelsea na Arsenal
Usajili wa dirisha dogo mwezi january itakuwa changamoto kwa timu za Man United, Chelsea na Arsenal
Siku tano pekee ndio zimesalia kabla ya ulimwengu wa soka kuuaga mwaka 2013 na nyakati kama hizi stori kubwa huwa tetesi za usajili wa wachezaji ambao baadhi ya makocha kwenye timu kuwa wanataka kuwaongeza kwenye timu zao ili kuboresha na kuongeza kiwango kitakachowafanya wapate mafanikio wanayoyasaka .
Ni kipindi cha mwezi januari ambapo dirisha dogo la usajili hufunguliwa kwa muda wa mwezi mzima na kutoa fursa kwa timu kufanya usajili wa wachezaji wapya .
Klabu ya Manchester United inatarajiwa kuwa moja ya timu zitakazotumia fedha nyingi mwezi wa januari kutokana na mapungufu ambayo kocha David Moyes ameyaona na haishangazi kuwa timu hii ndio inayoongoza kwenye tetesi za usajili.
Mmoja wa wachezaji waliohusishwa na usajili kwenye kikosi cha United ni kiungo wa Hispania Koke ambaye anacheza kwenye klabu ya Atletico Madrid .
United huenda ikamnunua kiungo huyo kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 30 baada ya David Moyes kufunga safari hadi nchini Hispania kumtazama mara zaidi ya moja.
Jina lingine ambalo limehusishwa na United ni jina la kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Marco Reus ambaye klabu yake ya Borrusia Dortmund imeiambia United iwalipe paundi milioni 40 endapo itataka kumnunua . United pia wamehusishwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Brazil Everton Ribeiro anayechezea klabu ya Cruzeiro ya huko Brazil.
Arsenal wametajwa kuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Mitchy Batshuayi anayechezea klabu ya Standard Liege .
Arsenal kwa sasa wamekuwa wakimtumia mshambuliaji mmoja pekee ambaye ni Olivier Giroud huku akisaidiwa na Nicklas Bendtner na kwa kiasi kikubwa hitaji la klabu hii toka London kwenye dirisha la usajili ni mshambuliaji ambaye atakuwa akitoa changamoto kwa Giroud .
Chelsea nao kwa hakika hawatakuwa nyuma kwenye “shopping” ya dirisha dogo la usajili na kama Arsenal mahitaji yao makubwa yatakuwa kwenye idara ya ushambuliaji.
Radamel Falcao wa As Monaco na Jackson Martinez wa Fc Porto wametajwa kuwa kwenye mipango ya Jose Mourinho huku jina la kiungo wa Inter Milan Freddy Guarin nalo likitajwa.
Jackson Martinez Mcolombia anayechezea Fc Porto ni chaguo la pili baada ya Falcao kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Chelsea.
Usajili wa dirisha dogo mwezi january itakuwa changamoto kwa timu za Man United, Chelsea na Arsenal
Reviewed by bongohitz1
on
1:29:00 PM
Rating: 5
No comments