Matokeo ya Ligi ya England kwa michezo ya ‘Boxing Day’.
Ligi kuu ya England imeshuhudia viwanja 10 vikitoa burudani ya soka kwenye siku ya kufungua ‘maboksi’ ya zawadi za Krismasi yaani Boxing day ambapo timu zote 20 za ligi hiyo zilikuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Mchezo wa kwanza ulipigwa kwenye uwanja wa KC ambako Manchester United walishinda mchezo wao wa 5 mfululizo baada ya kuwafunga Hull City 2-3 .
Nyota wa mchezo huo alikuwa Wayne Rooney ambaye alifunga bao la kusawazisha baada ya United kujikuta ikiwa nyuma kwa mabao mawili yaliyofungwa ndani ya dakika 13 za kwanza .
Bao la pili la Rooney lilimfanya afikie rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ya kufunga mabao 150 kwenye timu moja .
Wafungaji wengine kwenye mchezo huo walikuwa James Chester David Meyler kwa upande wa Hull City huku mchezaji aliyefunga bao la kwanza la mchezo huo James Chester akiifungia United bao la ushindi baada ya kujifunga mwenyewe akiwa kwenye harakati za kuokoa , bao hilo lilifungwa baada ya Chris Smalling na Wayne Rooney kuirudisha United mchezoni .
Arsenal walifanikiwa kurudi kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuwafunga West Ham United kwa 3-1 . Wafungaji wa Arsenal walikuwa Theo Walcott ambaye alifunga mabao mawili na Lukas Podolski ambaye alifunga bao lake la kwanza tangu arudi toka alipoumia na kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu na bao pekee la West Ham lilifungwa na mshambuliaji Carlton Cole likiwa bao lake la pili mfululizo baada ya kufunga jumamosi iliyopita kwenye mchezo dhidi ya Man United.
Liverpool ambao walikuwa wakiwania kurudi kileleni mwa ligi walipoteza mchezo wao dhidi ya Manchester city kwa matokeo ya 2-1 . Liverpool walianza kufunga kupitia kwa Felipe Coutinho kabla ya Vincent Kompany na Alvaro Negredo hawajaifungia City mabao yaliyowapa pointi tatu muhimu.
Matokeo ya michezo ya leo yanamaanisha kuwa Arsenal wanaongoza ligi wakiwa na pointi 39 wakifuatiwa na Chelsea wenye pointi 37 , Liverpool wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 36 na Man City wanakamilisha “Top 4’ wakiwa na pointi 35.
Matokeo ya Michezo ya Tarehe.26/12/2013.
Hull City 2-3 Man United .
West Ham United 1-3 Arsenal .
Everton 0-1 Sunderland .
Newcastle United 5-1 Stoke City.
Norwich City 1-2 Fulham .
Aston Villa 0-1 Crystal Palace.
Cardiff City 0-3 Southampton.
Tottenham 1-1 West Brom
Manchester City 2-1 Liverpool.
Matokeo ya Ligi ya England kwa michezo ya ‘Boxing Day’.
Reviewed by bongohitz1
on
1:25:00 PM
Rating: 5
No comments