Recent comments

Breaking News

STAR MKENYA KWENYE ’12 YEARS A SLAVE’ HAKUHUDHURIA UZINDUZI WA FILAMU HIYO KWA SABABU YA UBAGUZI?

Mrembo wa Kenya Lupita Nyong’o ambaye ameigiza kama star kwenye filamu ya Hollywood ‘12 Years a Slave’ iliyomkutanisha na waigizaji maarufu akiwemo Brad Pitt, hakuonekana kwenye uzinduzi wa filamu hiyo jana (December 27).
Kutohudhuria kwake kwenye uzinduzi wa filamu hiyo kumeunganishwa na suala la ubaguzi wa rangi uliojitokeza katika posters za filamu hiyo ambazo zinawaonesha waigizaji ‘wazungu’ na kumuweka pembeni Lupita Nyong’o ambaye amechukua nafasi kubwa katika filamu hiyo.
Hata hivyo msemaji wa kampuni ya Lionsgate wanaohusika na uuzaji wa filamu hiyo, amesema kuwa kutoonekana kwa Nyong’o katika uzinduzi huo hakuna uhusiano na utata uliojitokeza katika posters za filamu hiyo.
Amesema kuwa muwakilishi wa Nyong’o aliwaambia waandaaji wa tukio hilo wiki mbili kabla kuwa muigizaji huyo asingehudhuria.
Posters zilizotolewa zimeonesha ubaguzi baada ya kuwaweka pembeni waigizaji wengine ambao wamechukua nafasi kubwa katika filamu hiyo kama Lupita Nyong’o na Chiwetel Ejiofor, na badala yake wameonekana Brad Pitt na Michael Fassbender.
Hata hivyo Summit Entertainment waliomba radhi kwa posters hizo na kudai kuwa hazikuwa zimeruhusiwa na uongozi, na hivyo kupiga marufuku usambazaji wa posters hizo.

No comments