Recent comments

Breaking News

MANDELA: LONG WALK TO FREEDOM YAPATA NOMINATIONS 3 GOLDEN GLOBE…

Sinema ya Mandela: Long Walk To Freedom, ni sinema ambayo inaelezea maisha ya Rais wa kwanza wa South Africa, Nelson Mandela na harakati zake za kupigania haki sawa, pamoja na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo…
Sinema hii imefanikiwa kupata nomination 3 katika tuzo za Golden Globe ambapo nominations za tuzo hizo zilifanyika mwezi huu katika jiji la Los Angeles huko Marekani.
Sinema hiyo imefanikiwa kumtoa muigizaji mahiri Idris Elba kuwania tuzo ya Best Actor – Motion Picture Drama, ambapo muigizaji huyu aliigiza kama Nelson Mandela katika sinema hiyo. Pia Alex Heffes atawania tuzo ya Best Original Score kupitia sinema hiyo ikiwa ni nomination ya pili na nomination ya tatu ilikwenda kwa kundi la music/Band la miondoko ya Rock .. U2 kwenye category ya Best Original Song – “Ordinary Love” ambapo wimbo huu ulitungwa special kwa ajili ya Nelson Mandela.

No comments