Recent comments

Breaking News

MJOMBA KUIZINDUA RASMI STUDIO YAKE YA ‘WAITE RECORDS'

Mrisho Mpoto aka Mjomba ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya poa sana katika soko la muziki hapa Tanzania, kutokana na uwezo wake wa kutunga na kughani mashairi kupitia nyimbo zake mbalimbali kama vile ‘Adela’ ‘Chochea Kuni, ‘Salamu’ nk.
Siku ya kesho Mjomba anatarajia kuzindua rasmi studio yake iliyopo Kinondoni Mkwajuni, ni studio ya kisasa zaidi na kutakuwa na utambulisho wa wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la ‘Waite’ aliyoufanyia katika studio yake.
Sherehe itaanza majira ya saa moja jioni katika maeneo ya ofisi yake Kinondoni Mkwajuni, na mgeni rasmi anatarajia kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Jerry Slaa pamoja na viongozi mbalimbali watakuepo.
Picha za ndani za studio hiyo:
Mjomba9
Mjomba-7
Mjomba-6

No comments