Recent comments

Breaking News

DJ CHOKA KUTOFANYA U-DJ MWAKA 2014…?

Dj Choka ni mmoja kati ya Ma-dj wachache nchini ambao wana sifa ya ucheshi na kutamaniwa na wasanii wengi wafanye nao kazi huku akiwa ndiye DJ wa kwanza kufanya ngoma zake mwenyewe akiwashirikisha wasanii wengine na kuziingiza sokoni zikabamba industry hii ya Bongo Fleva.
Tukiwa tunaenda mwishoni kabisa mwa mwaka huu wa 2013, DJ CHOKA amewastua wengi kwa kuandika hiki kwenye page yake ya facebook..
“Tokea niingie kwenye game la mziki..sijawahi kupata manufaa yoyote nikimaanisha labda mziki umenilipa chochote au umeninufaisha. Nikimaanisha hakuna kipato kikubwa anacholipwa DJ hapa Tanzania kama haujaonyesha juhudi zako au kujituma. Kwa mimi nimeangaika usiku kucha kulala ni kidogo sana ili tu nije kupata hichi kidogo ninachokitafuta. Lakini kusema ukweli kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu BLOG/WEBSITE yangu ndio inayonipa faraja na moyo wakujituma na ndio inayoendesha maisha yangu na malezi bora kwa familia yangu kutokana na matangazo ninayoyapata. 2013 Ulikuwa mwaka mgumu sana kwangu lakini nimepiga nao hadi leo naishi hivyo hivyo kama kumsukuma mlevi bora afike nyumbani. Soon nitatangaza kipi nitapumzika na kuendelea na kitu kimoja katika maisha yangu ambacho naona kitanilipa zaidi, najua nitawakwaza ila ndio maamuzi nitakayoyafanya kwamaana naamini wako wengi wanaotaka kuwa kama mimi so lazima niwape nafasi hiyo ili tuwe vijan a wengi wachapakazi kuliko kila kitu nifanye mimi NIKIFA JE. Napenda kuwashukuru VODACOM TANZANIA kwa matangazo maana wao ndio wameendelea kuwa na me mpaka hapa na kujivunia kuwa mtu katika watu. HAPPY NEW YEAR 2014″

No comments