Tuesday, June 19, 2012

SEHEMU YA MAPENDEKEZO YA BAJETI MBADALA YA KAMBI YA UPINZANI.

MH.ZITO KABWE (KIGOMA-CHADEMA)
Zitto Kabwe.
Kambi rasmi ya upinzani bungeni imewasilisha bajeti mbadala ya kambi hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na kuitaka serikali kuwa makini katika kukopa nje ya nchi kutokana na kukua kwa kasi kwa deni la taifa na kupendekeza pia magari ya kifahari ya serikali yapigwe mnada ili kupunguza matumizi ya mafuta.
Pamoja na hizo ishu kambi hiyo imeitaka serikali kuainisha njia za kudhibiti mfumuko wa bei unaowaongezea mzigo wananchi na kuwaongezea mishahara walimu, madaktari na wauguzi kwa asilimia 50 huku ikiweka mpango wa kuanza kuwalipa pensheni wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa ruhusa ya Chadema Zitto Kabwe ambae pia ni waziri kivuli wa fedha amesema “swala ni kwamba tunakopa ili kufanya nini? bajeti ya mwaka 2012/2013 inayopendekezwa inaonyesha kwamba serikali itakusanya trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida, ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida, hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya posho”
Kabwe amekamilisha kauli yake akikaririwa akisema “tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi, kuiacha serikali kuendelea kukopa bila mpango ni kuliweka taifa rehani, hatuwezi kukubali wazee wetu waishi maisha yao waishi maisha yetu na wakope maisha ya watoto wetu”
Wabunge mbalimbali walichangia bungeni Dodoma June 18 2012 na kulalamikia kuongezeka kwa deni la taifa, usimamizi mbaya wa rasilimali za nchi na ugumu wa maisha kwa mtanzania na wengine wakakataa kuiunga mkono bajeti hiyo.

No comments:

Post a Comment