Recent comments

Breaking News

Video: Eviction Night Oneal (Shemejiiiii) akiyaaga mashindano ya BBA jana usiku Feza Aishukuru Africa

Jana (August 4) Africa ilionyesha furaha kwa mshiriki wa BBA Tanzania, Feza Kessy baada ya kumsave na kuendelea kubaki katika mashindano hayo. Feza ambae alionekana kukata tamaa alionyesha furaha hiyo mara baada ya kutangazwa kutoka kwa mpenzi wake "Oneal" (Botswana) ambae nae alikuwa amekaa nae kwenye kuti kavu.

"phweeeeeeee thank you Africa" alionekana akisema Feza mara baada ya kumsindikiza mpenzi wake mlangoni

Feza alipigiwa kura na nchi tatu ambazo ni Tanzania. Kenya na Sierra leone, ambapo Oneal alipata kura mbili kwa kupigiwa kura na nchi yake Botswana na South Africa, na hivyo kumsababishia kuyaaga mashindano hayo.

Bimp (Ethiopia) ambae pia alikuwa katika eviction ali prove kukubalika na Africa kwa kupigiwa kura 10 kutoka katika nchi kumi tofauti ambazo ni Angola, Ghana, Ethiopia, Namibia, Malawi, Nigeria, Uganda, Zambia, Zimbabwe na nchi zingine za Africa zilizosalia

Zimebaki siku 20 tu kukamilika kwa siku 90 za kufikia fainali ya mashindano hayo, ambapo ni washiriki 5 tu ndio watakao ingia katika fainali hizo ( wamebaki 8 sasa), endelea kumpigia kura Feza Kessy mara nyingi uwezavyo 

No comments