Home
/
Unlabelled
/
Picha zaidi ya 20 za ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi ya kasi Jangwani – Kimara. "Kwa hisani kubwa ya mtu wangu wa nguvu Bw. Millard Ayo"
Picha zaidi ya 20 za ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi ya kasi Jangwani – Kimara. "Kwa hisani kubwa ya mtu wangu wa nguvu Bw. Millard Ayo"

Kutokana na foleni kubwa ambayo imekuwa tatizo kwa wakazi wa Dar es salaam hasa wenye shughuli zinazowalazimu kufika mjini, serikali ilianzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi ikiwa ni moja ya mipango ya kuepusha foleni.
Huu mradi umeanza na ujenzi ambao unaweza kuonekana hasa kwenye barabara ya Morogoro, hii hapa ni update jinsi mradi huo unavyoendelea hivi sasa kuanzia stendi kuu pale Jangwani hadi Kimara mwisho.

Ukiwa bar au restaurant, hii ndiyo view yako ambayo ni parking ya mabasi yenyewe ambapo basi likifika unaenda zako kupanda

Haya mabomba yanatumika kujenga mfumo mzuri wa maji taka kwasababu mitaro mingi imefukiwa ili barabara ijengwe.

Ukitoka Jangwani ukafika mbele kidogo Magomeni Usalama kituo kimeshawekwa hadi kibao cha utambulisho.

Mtu wangu wa nguvu hapohapo Magomeni pia kuna tawi la NMB Bank, unaweza kufika na kujipatia huduma za kibenki pia.

Vituo vya haya mabasi ni virefu kama unavyoona mwenyewe ambapo basi litakua linapaki kwa pembeni alafu ndani ya hizo chuma ndio kutakua na viti na vioo kwa ajili ya abiria kupumzika na kusubiri basi.

Safari ilifika Manzese, huu ni muonekano wa maendeleo ya barabara kutoka kwenye daraja la Manzese na kituo kinaonekana kwa mbali.

Safari ikafika Ubungo, kuna vitu vinafanyika kwenye huu ujenzi kwa mtu ambaye sio mtaalamu au haujaiona ramani ya ujenzi huu sio rahiis kuelewa ni nini wanafanya, mfano hapa sikupata hata mwenyeji wa kunielezea ni kitu gani hiki.

Hiki ni kitu kama daraja kinajengwa na mara ya mwisho napita hapa halikuwepo, leo nimeona mabadiliko.
Use Facebook to Comment on this Post
Picha zaidi ya 20 za ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi ya kasi Jangwani – Kimara. "Kwa hisani kubwa ya mtu wangu wa nguvu Bw. Millard Ayo"
Reviewed by bongohitz1
on
5:25:00 AM
Rating: 5
No comments