Recent comments

Breaking News

MISS TZ: KWENDA INDONESIA SEPTEMBER.

Miss Tz 2012/2013 Brigitte Alfred anaendelea na maandalizi ya mashindano ya Miss World yatakayofanyika Indonesia Sept, 28 mwaka huu.
Mrembo wa Tanzania akiwa ni mtu mwenye kujiamini na kile anachoenda kukifanya katika mashindano ya Miss World na kujiamini kwake kumepelekea watanzania kuamini ushindi ni wetu.
Mwakilishi wa Tanzania anarajia kuondoka mwanzoni mwa mwezi septemba kwenda nchini Indonesia katika kambi ya Miss World.

Miss Tz Brigitte Alfred baada ya kuitikia wito wa kuja katika ofisi ya Baabkubwa Magazine na kufanya interview kuhusiana na maandalizi ya safari yake pamoja na kutwaa taji la Miss World 2013 alisema

“Preparation zipo, nina andaliwa vizuri kwa ajili ya kwenda kushindana nia na lengo ni kushinda taji la Miss World na hiyo yote inatokana na my confidence, so still na muomba Mungu pamoja na jitihada zangu ili niiwakilishe vyema nchi yangu”.
Katika kinyanganyiro cha kumtafuta Miss World 2013 kuna Warembo 96 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni,Baabkubwa Magazine inamtakia kila la kheri Miss Tz katika maandalizi ya kujiandaa na kinyanganyiro cha Miss World.

No comments