HUU NDIO UKWELI KUHUSU ANGELINE JOLIE (MUIGIZAJI WA FILAMU MAARUFU DUNIANI) KUONDOA MATITI YAKE.

Moja ya Habari kubwa kwenye mitandao toka jana ni kuhusu mwigizaji wa kike maarufu Angeline Jolie ambaye ni mke wa mwigizaji Brad Pitt kukatwa matiti.Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.

Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Angeline Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa uwezekano wake kupata
Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake
wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
No comments